Entertainment

Catherine Kusasira awaasa wasanii wa kike Uganda kujitengana na matumizi ya vipodozi

Catherine Kusasira awaasa wasanii wa kike Uganda kujitengana na matumizi ya vipodozi

Mwimbaji wa bendi  Catherine Kusasira amewapa somo wasanii wa kike nchini Uganda kujiepusha na matumizi ya vipodozi kwenye miili yao.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Kusasiri anasema vipodozi ina kemikali hatari ambayo inazeesha ngozi haraka.

Hitmaker huyo wa “I Love You” anadai kuwa hatumii vipodozi usoni mwake mbali na mafuta aina ya Vaseline.

“Situmii vipodozi na ninawashauri waimbaji chipukizi kujiepusha kutumia kemikali kama hizo kwenye nyuso zao. Situmii vipodozi na ndio maana naonekana mdogo kila mara unaponiona,” alisema katika mahojiano na runinga moja nchini Uganda.

Kusasira amesema alipata msukumo wa kuzingatia urembo wa asili kutoka kwa wasanii wakongwe nchini humo Mariam Ndagire na Neema Nalubega.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *