
Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Jose Chameleone amefunguka tusiyoyajua kuhusu maisha ya msanii aligeukia siasa Bobi Wine.
Kwenye moja ya performance yake juzi kati, Chameleone amedai kwamba Bobi Wine hawezi tena toka nje ya ndoa yake kwa sababu anaogopa kuwekewa sumu.
Hitmaker huyo wa Bolingo ya Nzambe amesema Bobi Wine anahofia sana wanawake kwa kuwa wanaweza tumiwa na watesi wake kumuangamiza.
“Bobi Wine alikuwa jambazi kama mimi lakini sasa hawezi tena kufurahia maisha ya usiku jijini Kampala. Hata aliomba usalama kutoka kwa vyombo vya usalama kuhudhuria tamasha la Fik Fameika. Anaogopa kufanya mapenzi na wanawake wengine kwa sababu anaweza kulishwa sumu,” alisema. .
Mwimbaji huyo ameongeza kuwa Bobi Wine anakosa maisha yake ya muziki ambayo yalikuwa yanampa huru wa kutangamana na mashabiki bila uoga wowote.