Entertainment

Chameleone Ashauriwa Akabidhi Nyumba na Mali kwa Daniella

Chameleone Ashauriwa Akabidhi Nyumba na Mali kwa Daniella

Aliyekuwa mbunge, Mubarak Munyagwa, ameibuka na ushauri kwa msanii nyota wa Uganda, Jose Chameleone, akimtaka akubaliane na masharti yote yaliyowekwa na mkewe, Daniella Atim, katika mchakato wa talaka yao.

Munyagwa amesema kuwa Chameleone ni msanii mwenye juhudi na uwezo wa kujenga au kununua nyumba nyingine, hivyo hana sababu ya kushikilia mali hiyo. Aidha, amesisitiza kuwa kukubali hata ombi la Daniella la kupata asilimia 60 ya mali ya Chameleone kutaleta amani na kulinda heshima ya familia.

Kwa mujibu wa Munyagwa, Chameleone hafai kuonyesha hasira wala upinzani dhidi ya watoto wake kwani hali hiyo inaweza kuwafanya wamchukie kwa kutowelewa hali ilivyo.

Hata hivyo, upande wa Chameleone umekuwa na msimamo tofauti. Ingawa yuko tayari kukubali talaka, amekuwa akipinga baadhi ya masharti ya Daniella, hasa kuhusu nyumba ya familia iliyoko Sseguku na malezi ya watoto. Mwanamuziki huyo anataka nyumba ibaki mali ya familia na malezi yawahusishe wote wawili badala ya Daniella pekee.

Daniella, kwa upande wake, ameomba mahakama impe malezi kamili ya watoto wao, umiliki wa nyumba ya Sseguku, pamoja na fedha za matumizi ya kila mwezi kwa ajili yake na watoto. Pia amedai asilimia 60 ya mali za Chameleone ili kufanikisha maisha ya familia yake baada ya talaka hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *