Entertainment

CHAMELEONE AWAPA SOMO MASHABIKI

CHAMELEONE AWAPA SOMO MASHABIKI

Lejendari wa muziki kutoka nchini Uganda Jose Chameleone amewapa somo mashabiki wanaomkosoa kwa kufanya kazi na serikali ya rais Yoweri Museveni.

Katika performance yake katika kumbukiza ya General. Muhoozi huko Cricket Oval, Lugogo chameleone amedai kuwa hatokubali kuvunjiwa heshima na mashabiki wanaomtaka afuate wanachokisema mtandaoni kwa kusema kwamba yeye ni mtu mzima na hawezi kupangiwa maisha.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Bei Kali” amesema hajali tena namna watu wanavyomchukulia kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa tayari ameshastaafu siasa.

Inaripotiwa kuwa Chameleone na Bebe Cool ndio wasanii waliolipwa mkwanja mrefu kwenye hafla ya kumbukizi ya General. Muhoozi ambaye ni mwanawe Yoweri Museveni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *