Entertainment

Cheed na Killy waondoka rasmi Konde Gang

Cheed na Killy waondoka rasmi Konde Gang

Lebo ya Konde Music Worldwide inayomilikiwa na Harmonize imetangaza rasmi kusitisha mkataba na wasanii wake wawili Cheed na Killy kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao.

Lebo hiyo ambayo leo imetimiza miaka 4 tangu kuanzishwa kwake Oktoba 10, mwaka 2019, iliwasajili Cheed na Killy Septemba mwakaa 2020 wakitokea lebo ya King’s Music ya Ali Kiba

Wasanii hao wanaungana na rapa Country Boy ambaye alijitoa Konde Music mapema mwa mwaka huu.

Kwa miaka miwili waliyokuwepo Konde Music,Killy aliweza kutoa Greenlight EP yenye jumla ya nyimbo 5 huku Cheed akiachia Endless love EP yenye jumla ya ngoma 6 za moto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *