Bilionea maarufu mtandaoni, Chief Godlove, amewaziba mdomo watu waliomcheka kufuatia taarifa zilizosambaa mitandaoni zikidai magari yake yalipigwa mnada kutoka na madeni.
Kupitia ujumbe wake mzito, amejigamba kuwa hatafilisika milele kwa kuwa bado ana uwezo mkubwa kifedha. Amesisitiza kuwa hakuna mtu yeyote anaweza kumwambia chochote kuhusu maisha au mafanikio.
Godlove amesema kejeli alizopokea zimemfungua macho na kumfundisha funzo kubwa kwamba watu wengi hawafurahii mafanikio ya wengine, hasa pale mtu anapofanikiwa kwa kasi. Ameeleza kuwa badala ya kuonea fahari hatua alizofikia, baadhi ya watu wamekuwa wakisubiri anguko lake ili wapate jambo la kucheka.
Chief Godlove ameenda mbali zaidi kwa kuwashambulia waliomcheka, akiwaita maskini, akisema kejeli zao zinatokana na chuki na wivu. Amehitimisha ujumbe wake kwa kusisitiza kuwa ataendelea kusonga mbele, kufanya kazi na kufanikisha malengo yake bila kujali maneno ya watu.