Entertainment

CHIMANO WA SAUTI SOL AUMIZWA NA KITENDO CHA POLISI KUSITISHA TAMASHA LA “LOVE & HARMONY”

CHIMANO WA SAUTI SOL AUMIZWA NA KITENDO CHA POLISI KUSITISHA TAMASHA LA “LOVE & HARMONY”

Member kundi la Sauti Sol Willis Austin Chimano amesikitishwa na hatua ya tamasha lake la “Love and Harmony” kusitishwa na maafisa wa usalama.

Kupitia Instagram page yake Chimano, amewalaumu maafisa wa polisi kutokana na kile alichokitaja kuwa na ubaguzi ikizingatiwa kuwa awali tamasha hilo lilikuwa lifanyika katika eneo la Westlands, Nairobi lakini polisi walimshauri abadili eneo kutokana na sababu za kiusalama.

Msanii huyo ameenda mbali zaidi na kusema kuwa licha ya kuridhia na kubadili eneo la tamasha hadi barabara ya Ngong, Jijini Nairobi maafisa wa polisi wamefutilia mbali  onesho la “Love and Harmony”  kwa mara nyingine.

“Wanyanyasaji huwa hawaibuki washindi! Huenda mmefaulu zamu hii. Mmenitia ari zaidi. Tamasha ambalo nimeandaa kwa muda mrefu lazima lifanyike.” ameandika Chimano.

Chinamo amedai kwamba polisi wamechukua hatua hiyo kuzima uanaharakati wake wa kutetea haki za watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja huku akitoa hakikisho kwa mashabiki waliokuwa wamenunua tiketi za tamasha hilo kwamba watarejeshewa fedha zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa shirika la Bold Network Africa Makena Njeri amesema kwamba kama wadhamini walijaribu kutetea tamasha hilo lakini wakakutana na vizingiti vingi.

“Tulifanya bidii kutafuta eneo mbadala kama walivyoshauri lakini polisi wa Kenya wakatuagiza tusitishe tamasha bila maelezo yoyote.” ameandika Makena.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *