
Msanii na mcheza densi maarufu, Chino Kidd, amefunguka kuhusu changamoto anazopitia katika tasnia ya burudani. Staa huyo, anayejulikana kwa umahiri wake wa kucheza na pia sauti yake ya kipekee, amesema kuwa licha ya juhudi na historia ndefu ya kujituma, bado hajapewa heshima anayohisi anastahili.
Chino Kidd amesema safari yake imekuwa ngumu, ikianzia kwenye hustling za kila aina ili kutoboa kisanaa. Amedai kuwa wengi wanaufahamu mchango wake, hasa kwenye muziki na dansi, lakini mara nyingi anapuuzwa au kuonekana kana kwamba mchango wake hauna thamani kubwa.
Aidha, msanii huyo amesisitiza kuwa nia yake si kutafuta huruma, bali kutambulika kwa kazi na nidhamu yake. Anasema kuwa changamoto hizo hazijamvunja moyo, bali zinampa nguvu zaidi ya kusukuma muziki na dansi zake mbele, huku akiwataka mashabiki wake kuendelea kumuunga mkono.