Entertainment

CHOSEN BECKY AFUNGUKA JUU YA TETESI ZA KUFURUSHWA AFRIKA KUSINI

CHOSEN BECKY AFUNGUKA JUU YA TETESI ZA KUFURUSHWA AFRIKA KUSINI

Staa wa muziki nchini uganda Chosen Becky amekiri kwamba alifurushwa nchini Afrika Kusini kwa madai ya kukosa kibali cha kutumbuiza nchini humo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Chosen Becky kutimuliwa kwake nchini humo ilitokea mara baada ya maafisa wa serikali na hoteli aliyokuwa ameenda kukaa kutokuwa na maelewano mazuri.

Hata hivyo amewaomba radhi mashabiki zake wa Afrika kusini na kuhakikishia kwamba mapromota wanaifanyika kazi suala la yeye kutumbuiza nchini humo ambapo watangaza tarehe nyingine hivi karibuni.

Ikumbukwe Chosen Becky alipaswa kutumbuiza nchini Afrika kusini kati ya tarehe 6 na 13 mwezi wa Novemba lakini alifurushwa nchini kwao Uganda kutokana na kukosa kibali cha kutumbuiza nchini Afrika kusuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *