Entertainment

CHOSEN BECKY ATILIA SHAKA TUZO ALIYOPEWA NA MTN UGANDA

CHOSEN BECKY ATILIA SHAKA TUZO ALIYOPEWA NA MTN UGANDA

Msanii wa kike nchini Uganda Chosen Becky hajafurahishwa na hatua ya kampuni ya MTN kumtunuku tuzo ya wimbo bora wa bendi kwenye tuzo za Callers Tune.

Becky amesema hafanyi muziki wa bendi kama waandaaji wa tuzo walivyomchukulia ila anajihusisha na muziki wa Afro beat.

Hata hivyo hitmaker huyo wa ngoma ya “Party Time” amewashukuru waandaji wa tuzo za Callers tune na mashabiki kwa kumzingatia kwenye tuzo hizo.

Chosen Becky alishinda tuzo ya nyimbo bora ya bendi kupitia ngoma yake ya Nesimye ambapo alitunukiwa shillingi millioni 2.5 za Uganda.

MTN Callers tunes awards ni tuzo za kutambua mchangao wa wasanii ambao nyimbo zao zimepakuliwa zaidi kama callers tune.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *