Entertainment

Chris Brown Aahidi Kurejea Kwa Kishindo Kwenye Breezy Bowl Tour

Chris Brown Aahidi Kurejea Kwa Kishindo Kwenye Breezy Bowl Tour

Mwanamuziki nyota kutoka Marekani, Chris Brown, amevunja ukimya kwa mara ya kwanza baada ya kuachiwa kwa dhamana mapema leo, akieleza kuwa yuko tayari kuendelea na ratiba ya onyesho lake kubwa la Breezy Bowl linalotarajiwa kuanza Juni 13 jijini Manchester, Uingereza.

Kupitia ujumbe aliouweka kwenye mitandao ya kijamii, Chris Brown aliandika:

 “Kutoka kifungoni mpaka kwenye Jukwaa la Breezy Bowl,” kauli iliyowasisimua mashabiki wake duniani kote.

Taarifa za awali zilieleza kuwa msanii huyo alikumbwa na mkasa wa kuwekwa rumande kwa muda, hali iliyozua sintofahamu kuhusu mustakabali wa ziara yake ya kimuziki barani Ulaya. Hata hivyo, kwa mujibu wa ujumbe wake, Brown ameweka wazi kuwa yuko huru na amejipanga vilivyo kwa ajili ya tamasha hilo ambalo limekuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki.

Chris Brown, anayefahamika kwa uwezo wake wa kipekee wa kuimba, kucheza na kutumbuiza jukwaani, anatarajiwa kufanya maonyesho katika miji kadhaa barani Ulaya kupitia ziara ya Breezy Bowl, ambayo ni sehemu ya kampeni ya kuendeleza album yake ya hivi karibuni na kusherehekea mafanikio yake ya kimuziki.

Mashabiki nchini Uingereza na sehemu nyingine za dunia sasa wana kila sababu ya kuwa na matumaini kuwa tamasha hilo litaendelea kama ilivyopangwa, huku Chris Brown akiahidi kuwaletea burudani ya hali ya juu licha ya changamoto zilizojitokeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *