
Mwanamuziki kutoka Marekani Chris Brown amelipokea kwa mikono miwili Jina la Ki-Nigeria ambalo amepewa na raia wa Taifa hilo “Oluwa Gbenga Breezy” baada ya kukubali kushiriki kwenye nyimbo nyingi za wasanii wa Nigeria lakini pia kutumia lafudhi yao kwenye verse zake.
Kupitia insta story yake, Breezy amelipokea Jina hilo na kuonesha upendo kwa kuweka vikopa na emoji za kucheka.
Hivi karibuni Breezy amekuwa akifanya Kolabo na wasanii wa Nigeria ikiwemo Lojay X Sarz (Monalisa REMIX), Fireboy DML (Diana) lakini pia Wizkid na Davido ambao amekuwa akishirikiana nao kila uchao.