Entertainment

Chris Brown hawakataza mashabiki zake kuvaa bandana ya nyekundu

Chris Brown hawakataza mashabiki zake kuvaa bandana ya nyekundu
Mwanamuziki Chris Brown amesema na mashabiki zake ambao wanatarajia kuja kwenye ziara yake ya muziki ambayo ametangaza itaanza baadaye mwaka huu. Hakutaka kueleweka vibaya, hivyo akautumia ukurasa wake wa instagram kufafanua jambo kwamba, hataki mashabiki zake waje wakiwa wamevalia vitambaa vyekundu maarufu kama “Red Bandannas” kama ambavyo wanapeana hamasa ya kuvaa hivyo.
Breezy amewakataza mashabiki zake kufanya hivyo na kusema ni bora wavae Bandana za rangi ya Brown ili kutojiingiza kwenye matatizo.
Kwa historia, Kitambaa hicho chekundu kinaashiria upande wa “Bloods” kikundi maarufu nchini Marekani ambacho kinahusishwa na matukio ya uhalifu, dawa za kulevya, wizi wa magari, mauaji na mambo yote ya kihalifu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *