
Staa wa muziki kutoka Marekani Chris Brown ametupasha juu ya ujio wa Album yake mpya “Breezy”.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika Album hiyo itatoka mwezi Juni mwaka huu.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Go Crazy” hajaweka wazi orodha ya nyimbo wala wasanii walioshiriki kwenye album yake hiyo.
Hii itakuwa Album yake ya 10 ikiifuata Indigo iliyotoka mwaka 2019.