
Mwanamuziki wa bendi kutoka Uganda Chris Evans amepuzilia mbali madai kuwa ana mpango wa kutambulishwa nyumbani kwa msaniii mwenzake Mary Bata kama mume mtarajiwa wa msanii huyo kwa njia ya harusi ya kitamaduni.
Chris evans amesema ameshangazwa kuona barua ya mwaaliko ya harusi inayosambaa mtandaoni huku akisema kuwa barua hiyo ni batili kwani hana mpango wa kumtambulisha msanii huyo kwa wazazi wake.
Chris Evans amesema Mary Bata ni rafiki yake na ikitokea amemtambulisha kwa wazazi wake hawezi kataa ila kwa sasa hawana uhusiano wowote wa kimapenzi na mwanamama huyo.
“I didn’t know about this occasion. Mary Bata is my friend, if she chooses to introduce me, then I won’t refuse, but we don’t have such plans. I am not romantically involved with her. I don’t want to be embarrassed,” amesema Chris Evans.
Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wanahoji kuwa wawili hao walipanga tukio hilo kama njia ya kutangaza wimbo wao mpya uitwao Tubaale.