
Staa wa muziki kutoka nchini Marekani Chris Brown ameamua kuanika ushahidi wa sauti ya mwanamke aliyemfungulia mashtaka ya ubakaji anayefahamika kwa jina la Jane Doe
Mwanamke huyo alichukua headlines kwenye mitandao ya kijamii alipomtaka mwanamuziki huyo amlipe dolla milioni 20 kwa kile alichodai kuwa Chris Brown alimbaka kwenye Boti mwaka wa 2020.
Sasa Chris Brown Ameweka wazi sauti ya Mwanadada huyo kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram akimlalamikia kuwa kwanini hajibu text zake huku akimtaka waonane naye, kitu ambacho Breezy anaamini ni mchongo wa kutaka kumuharibia jina na sio kitu kingine.
“Unasoma SMS zangu na Bado hujaniblock nahisi Hunichukii Nataka tu kuonana na wewe tu tena ,Nijulishe kama unataka nikuache pekeako pia nitafanya,ila natamani tu kufanya mapenzi na wewe tena”..Sauti ya mwanamke huyo anasikika kwenye voice note aliyoshare Chris Brown kupitia Instagram Page yake.