Entertainment

Cindy ataka kukutana na Rais Yoweri Museveni

Cindy ataka kukutana na Rais Yoweri Museveni

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Cindy Sanyu amedokeza mpango wa kukutana na Rais Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kuzungumzia sheria ya hakimiliki.

Mwanamuziki huyo ameeleza kuwa amefanya mikutano na wabunge kuhusu utekelezwaji wa sheria ya hakimiliki lakini jitihada zake hazijazaa matunda yeyote.

“Muswada huu ulisainiwa kuwa sheria lakini haujaleta mabadiliko kwenyemuziki. Tunaamini Mheshimiwa Rais atatusaidia kwa sababu tumetembea ofisi mbali mbali lakini ni machache yamefanyika. Tunataka kukutana na Rais mwenyewe,” alisema katika mahojiano na runinga moja nchini uganda.

Cindy ni Rais wa Chama cha Wanamuziki Uganda (UMA), bodi inayowaleta pamoja wanamuziki tofauti nchini Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *