Entertainment

Cindy Sanyu aikataa bei ya mapromota kwa wasanii wa Uganda

Cindy Sanyu aikataa bei ya mapromota kwa wasanii wa Uganda

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Cindy Sanyu amepuzilia mbali bei ya kufanya biashara na wasanii iliyotolewa na chama cha mapromota nchini humo akiitaja kuwa batili.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Cindy amewataka wasaniii kutoitikia wito wa mapromota hao wabinafsi huku akiitaka chama cha mapromota nchini Uganda kufanya kazi na wasanii watakaomudu gharama zao.

“Kama huwezi kumudu msanii, usimpe kazi. Huwezi kumlazimisha msanii kujishusha kuendana na viwango vyako,” Cindy alisema.

Mapema wiki hii Chama Cha Mapromota nchini Uganda (National Promoters Association) walitangaza pesa watakazowalipa wasanii wao kwenye shows mwaka 2023.

Chama hicho kilieleza kuwa wamefanya utafiti na wameona umuhimu wa kuweka bei za wasanii wao ili kuendelea kufanya biashara na asiyefurahia malipo ya pesa walizowawekea wamewaruhusu kuandaa shows zao wenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *