
Staa wa muziki nchini Uganda Cindy Sanyu ameweka wazi matamanio ya kumaliza tofauti zake na wasanii wanaohisi kuwa ana ubaya nao mara baada ya Bebe Cool kudai kwamba msanii huyo ni dikteta.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Cindy Sanyu amesema yeye sio dikteta kama jinsi ambavyo baadhi ya wasanii wanamchukulia ila mwaka jana alihamua kuwakandia wasanii waliokuwa wanamshambulia sana kutokana na utendekazi wake katika muungano wa wanamuziki nchini Uganda.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Local Man” amedai kuwa kabla hajateuliwa kuwa rais wa muungano huo kwa mara pili ana mpango wa kuomba msamaha wasanii wote aliwakosoa kipindi cha nyuma.
Cindy ambaye anachuana na King Saha, Maurice Kirya pamoja na Daddy Andre kwenye wadhfa wa urais katika muungano wa wanamuziki ametoa wito kwa wanachama wa muungano huo kumpa kura zao kwenye uchaguzi ujao ili aweze kufanikisha mikakati aliyoanzisha kipindi anahudumu kama rais.