
Content creator kutoka Kenya, Commentator 254, amekataa kufichua chanzo cha kuachana na mama ya mtoto wake Moureen Ngigi baada ya kukaa pamoja kwa muda mrefu.
Akiwa kwenye channel yake ya YouTube, ameeleza kuwa ingawa amepokea maswali mengi kutoka kwa mashabiki wake kuhusu kilichosababisha kuvunjika kwa penzi lao baada ya miaka mitatu, hatatoa maelezo ya kina bila uwepo wa Moureen.
Kauli hiyo imeibua hisia mseto mitandaoni, mashabiki wengine wakihisi kuna zaidi ya kile kinachosemwa, huku wengine wakisifu uamuzi wake wa kuheshimu faragha ya aliyekuwa mpenzi wake.
Commentator 254 na Moureen Ngigi walikuwa moja ya wanandoa maarufu mtandaoni, wakijulikana kwa kushirikiana mara kwa mara kwenye maudhui ya YouTube na mitandao ya kijamii, hali iliyowafanya kujizolea mashabiki wengi.