
Staa wa Soka wa Ureno Cristiano Ronaldo amepokewa rasmi na ametambulishwa mbele ya mashabiki wa Club ya Al Nassr ya Saudi Arabia.
Ronaldo aliyejiunga na Al Nassr kama Mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba na Man United aliambatana na Familia yake kwa maana ya Watoto na Mpenzi wake Georgina Rodriguez.
Timu ya Al Nassr iliyomsajili Ronaldo na Club ya Newcastle ya England zinamilikiwa na Mmiliki mmoja na inadaiwa kuwa katika mkataba wa Ronaldo kuna kipengele cha kwenda Newcastle kwa mkopo kama watafuzu kucheza UEFA Champignons League.
Ronaldo, anakuwa mchezaji wa kwanza mwenye jina kubwa duniani kukipiga katika klabu hiyo kwenye historia ya maisha yake ya soka.