
Aliyekuwa mchezaji wa Manchester United, Cristiano Ronaldo atatambulishwa rasmi na klabu ya Al-Nassr mbele ya umati wa mashabiki katika uwanja wa Mrsool Park, unaomilikiwa na klabu hiyo uliyopo ndani ya jiji la Riyadh, Saudi Arabia ambao unaingiza mashabiki 25,000.
Ronaldo amewasili leo Saudi Arabia pamoja na familia yake akiambatana na watu wa mambo ya kiufundi na waandishi wa habari.
Ronaldo atakuwa mchezaji wa kwanza mwenye jina kubwa duniani kukipiga katika klabu hiyo kwenye historia ya maisha yake ya soka.
Vile vile waziri wa michezo wa Saudi Arabia Abdulaziz bin Turki Al-Feisal ameahidi atazisapoti klabu zote nchini humo endapo madili makubwa yatatokea.