Entertainment

DADDY ANDRE AMTEUA EMMA CARLOS KUWA MENEJA WAKE

DADDY ANDRE AMTEUA EMMA CARLOS KUWA MENEJA WAKE

Msanii kutoka nchini Uganda Daddy Andre amemteua meneja Emma Carlos kusimamia muziki wake upande wa shows.

Daddy andrea ambaye yupo chini ya Black Market Records amechukua hatua hiyo baada ya mapromota kulalamika kuwa amekuwa akikwepa baadhi ya shows zake jambo ambalo karibu limuaribie brand yake ya muziki.

Emma Carlos atatakiwa kuhakikisha anachukua maombi ya shows za msanii huyo lakini pia atafuatilia kwa ukaribu ratiba  zake ili aweze kutumbuiza kwenye shows zake zote bila kukosa.

Utakumbuka Emma Carlos ni moja kati ya mameneja wakongwe kwenye muziki nchini ikizingatiwa kuwa amesimamia kazi za wasanii wengi nchini akiwemo Coco Finger, Kalifah Aganagah Radio & Weasel na wengine wengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *