Entertainment

DAVID LUTALO AKERWA NA UKABILA ILIOKITHIRI UGANDA

DAVID LUTALO AKERWA NA UKABILA ILIOKITHIRI UGANDA

Msanii kutoka Uganda David Lutalo ameonekana kukerwa na tatizo la ukabila linaloendelea miongoni mwa wananchi nchini humo.

Kwenye tamasha lake la muziki lililomalizika wikiendi hii iliyopita Lutalo alilazimika kukatisha kwa muda kuwapa mashabiki burudani akiwa jukwaani na kuamua kuwapa somo waganda kuacha tabia ya kuwabaguana kwa misingi ya kikabila kwani hatua hiyo inarudisha nyuma nchini kimaendeleo.

Haikushia hapo alienda mbali zaidi na kuwapongeza wasanii wa uganda kuendelea kusaidiana kwenye shughuli za muziki huku akisisitiza kuwa hiyo ndio njia pekee ya kukuza na kuupeleka muziki wao kimataifa.

Mwishoni mwa juma lililopita David Lutalo aliandaa tamasha lake la muziki liitwalo “Kabisi Kadagala” tamasha ambalo lilipata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki na viongozi wakuu serikalini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *