David Lutalo Afichua Anapanga Kufanyia Mtoto Wake Uchunguzi wa DNA
Msanii nyota wa Uganda, David Lutalo, ameibua mjadala mkali katika tasnia ya muziki baada ya kufichua kuwa anapanga kumfanyia mtoto wake mmoja kipimo cha DNA kutokana na wasiwasi binafsi kuhusu uhalisia wa uzazi. Akizungumza katika mahojiano na YouTuber, Lutalo amesema kuwa amekuwa akiishi na mashaka kwa muda mrefu na anaamini kuwa matokeo ya kipimo hicho yatamsaidia kupata utulivu wa akili na amani ya moyo. Ameeleza kuwa uamuzi huo unatokana na hisia binafsi ambazo amekuwa nazo kuhusu baadhi ya mambo ya kifamilia, na anaamini majibu ya kipimo hicho yatasaidia kumtoa kwenye hali ya mashaka. Hitmaker huyo wa Kapapaala ameongeza kuwa kazi yao kama wasanii inawafanya kuwa mbali na familia zao kwa muda mrefu, jambo linaloweza kuathiri uaminifu katika mahusiano. Amefafanua kuwa mara nyingi wasanii hutumia wiki au hata miezi wakiwa kwenye ziara za muziki, hali inayowafanya wengine kutafuta uthibitisho wa mambo fulani muhimu kama uzazi kupitia vipimo vya DNA. Lutalo pia amefichua kuwa kutokuwa na imani kwa wanawake kumemfanya kuchukua hatua hiyo, akisisitiza kuwa ni bora kujua ukweli kuliko kuendelea kuishi na mashaka
Read More