Mchekeshaji maarufu mtandaoni Dem wa Facebook ameeleza kuwa hajui sababu kamili ya kusitishwa kwa kipindi chake cha kila wiki alichokuwa akiendesha na Oga Obinna, akisema uamuzi huo ulitokea ghafla bila maelezo yoyote rasmi.
Kwa mujibu wa Dem wa Facebook, wao walikuwa wakirekodi kipindi hicho kila Jumatatu, lakini wiki iliyofuata hakupokea ujumbe wowote kutoka kwa PA wa Obinna, hali iliyomfanya kuamini kwamba huenda kulikuwa na mabadiliko ya mipango au mtangazaji huyo aliamua kushika wasanii wengine mkono.
Akipiga stori na Podcast ya Mwakideu Live, amesema kuwa hakuwa amepokea taarifa yoyote ya kufutwa kwa show hiyo, na alitarajia kuwa wangeendelea kurekodi kama kawaida.
Kipindi hicho, ambacho kilikuwa kikipata umaarufu mkubwa kwa ucheshi na mijadala ya kijamii, kiliwavutia watazamaji wengi mitandaoni kutokana na utani na urafiki wa kipekee kati ya Dem wa Facebook na Oga Obinna.