Entertainment

Diamond Athibitisha Kuachia Albamu Mpya Mwezi Septemba 2025

Diamond Athibitisha Kuachia Albamu Mpya Mwezi Septemba 2025

Mwanamuziki nguli kutoka Tanzania, Diamond Platnumz, ametangaza rasmi kuwa albamu yake mpya inatarajiwa kutoka mwezi Septemba mwaka 2025. Akizungumza katika mahojiano maalum na jarida maarufu la Billboard, Diamond amesema maandalizi ya albamu hiyo yako katika hatua za mwisho.

Diamond Platnumz, ambaye ameendelea kuwa mmoja wa wasanii wakubwa barani Afrika, amesema sababu ya kuchelewa kutoa albamu mpya ni uhitaji wa ubora wa hali ya juu katika kila wimbo utakaokuwemo ndani ya Albamu hiyo. Ameeleza kuwa analenga kuhakikisha kila ngoma kwenye albamu hiyo ni hit, jambo linalohitaji muda mwingi wa kufanya utafiti, uandishi wa mashairi na utayarishaji wa muziki.

Kupitia mahojiano hayo, Diamond ameweka wazi kuwa hana haraka linapokuja suala la kutoa kazi ya muziki, kwani anaamini katika ubora kuliko haraka. Mashabiki wake wamepokea habari hizo kwa hamasa kubwa, wakisubiri kwa shauku ujio wa albamu hiyo ambayo inatarajiwa kuwa na ushirikiano wa kimataifa.

Albamu hiyo ya Septemba 2025 inatarajiwa kuwa moja ya kazi kubwa zaidi kutoka kwa Diamond Platnumz, na kuongeza mchango wake katika kukuza muziki wa Bongo Flava kwenye jukwaa la kimataifa.