Entertainment

Diamond Atoa Ujumbe wa Faraja na Amani Kwa Watanzania

Diamond Atoa Ujumbe wa Faraja na Amani Kwa Watanzania

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ameungana na Watanzania katika kipindi hiki cha huzuni na maombolezo kufuatia ghasia zilizoripotiwa baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, akisisitiza umuhimu wa imani, umoja na upendo miongoni mwa wananchi.

Kupitia ujumbe wake mtandaoni, Diamond alisema kuwa hakuna jambo hutokea bila mapenzi ya Mungu, akiongeza kuwa kila tukio lina sababu ya kimungu inayoweza kuleta baraka na mafanikio kwa taifa endapo watu watadumisha amani na mshikamano.

Msanii huyo amewataka Watanzania kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu ili awajaalie amani zaidi ya waliyoipata hapo awali, upendo, umoja, na maendeleo kwa wote. Amemaliza ujumbe wake kwa kuwaombea waliopoteza maisha wapumzike kwa amani na kwamba taifa lipate faraja na nguvu ya kusonga mbele kwa matumaini mapya.

Kauli ya Diamond inakuja baada ya tetesi kusambaa mtandaoni zikidai kuwa Diamond na familia yake waliondoka nchini Tanzania kwa hofu ya kushambuliwa, baada ya baadhi ya biashara za wasanii waliomuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kuripotiwa kushambuliwa na waandamanaji waliopinga uchaguzi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *