Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, amewahimiza vijana kutokata tamaa katika maisha na badala yake waendelee kuweka juhudi ili kufikia malengo yao.
Akizungumza baada ya Mama Asha Baraka kuteuliwa kuwa Mbunge Maalum, Diamond amesema uteuzi huo ni ushahidi kuwa juhudi na uvumilivu huzaa matunda, kwani Mama Asha amesimama mara 20 bila mafanikio katika chaguzi zilizopita.
Mkali huyo wa ngoma ya Msumari, amesema vijana wanapaswa kujifunza kutokana na mfano wa Mama Asha Baraka, ambaye licha ya kushindwa mara nyingi, hakuwahi kukata tamaa hadi akatambuliwa na kuteuliwa kushika nafasi hiyo ya heshima.
Diamond amesisitiza kuwa mafanikio hayaji kwa urahisi na kwamba kila changamoto ni sehemu ya safari ya mafanikio.