
Mwanamuziki wa Bongofleva Diamond Platinumz ameachia rasmi EP yake ya First Of All iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.
First Of All Ep ina jumla ya nyimbo 10′ ya moto ikiwa na kolabo 5 ambazo mbili kati ya hizo amefanya na wasanii wake kutoka WcB mbosso na zuchu ,huku akitoa shavu kwa mwanamuziki wa nigeria adekunle gold katika track namba 5 , track namba 10 akiwashirikisha wakali kutoka Afrika kusini na track namba 1 akimshirikisha msanii Jay Willz.
Ep hiyo ambayo ni kwanza kwa mtu mzima Diamond Platinumz ina nyimbo kama Somebody, Fine, Melody, Sona, Loyal, Wonder, Mtasubiri, Fresh na Inapatikana Exclusive kupitia digital platforms mbali mbali za kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni.