Entertainment

DIAMOND PLATINUMZ APEWA JEZI NA TIMU KUBWA USA

DIAMOND PLATINUMZ APEWA JEZI NA TIMU KUBWA USA

Msanii mwenye tuzo nyingi zaidi Afrika Mashariki na Kati Diamond Platnumz amepewa heshima kubwa na timu ya Mpira wa Marekani inayofahamika kama washington NFL.

Diamond amekabidhiwa jezi namba 99 huku ikipambwa na jina lake mgongoni Platnumz.

Timu hiyo ambayo inashikilia nafasi ya pili kwenye Ligi ya mpira wa Marekani imechapisha picha hizo za Diamond kwenye ukurasa wao wa Instagram na kuandika “diamond platnumz repping the Burgundy & Gold”

Diamond Platnumz anakuwa msanii wa pili kutoka bara la Afrika kukabidhiwa Jezi na timu kubwa za mpira duniani baada ya siku chache zilizopita burna boy kupewa jezi na klabu ya Manchester United

Diamond kwa sasa yupo nchini Marekani kwaajili ya ziara ya kimuziki ambapo mpaka sasa ameshatumbuiza kwenye miji miwili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *