
Mwanamuziki kutoka nchini Tanzania Diamond Platnumz amekosolewa mitandaoni kwa kutumia bendera yenye utata katika video ya wimbo wake mpya wa Gidi.
Moja ya kipande cha video katika wimbo wa Gidi kina bendera mbili za kibaguzi wa rangi zinazoonyeshwa wakati Diamond akicheza huku nyingine akiwa na muonkeano wa Cowboy.
Bendera hiyo ni ya kundi la Shirikisho la majimbo ya kusini ya Marekani ambayo yalipigania kudumisha utumwa wa watu weusi kati ya mwaka wa 1960 na 1961 na inaonekana kama ishara ya mivutano ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani.
Jambo hilo limezua gumzo mtandaoni ambapo watumiaji wengi kwenye mitandao ya kijamii hasa wafrika wameshambulia Diamond Platinumz kwa hatua ya kutumia bendera hiyo ya kibaguzi kwenye video ya wimbo wake Gidi kwa sababu ina tafsiri ya moja kwa moja kwamba ameungana na wazungu katika kuwapiga vita ndugu zake Weusi.
Hata hivyo wamemshauri msanii Diamond pamoja na uongozi wake kuhariri upya video hiyo na kutoa sehemu ambazo zina muonekano wa bendera hiyo kwani hili litakuwa jambo zuri tena la busara kwa msanii kama yeye ambaye analenga kupenya katika soko la muziki la Marekani.