
Wakati ambao EP mpya ya msanii Diamond Platnumz “First of All” ikiendelea kufanya vizuri kwenye digital Platforms mbalimbali, Habari njema kwa mashabiki wa nyota huyo ni kwamba, Ijumaa hii anatarajia kuonekana ndani ya jukwaa la Netflix kupitia reality show ya “Young, Famous and African” ambayo inaanza rasmi Machi 18.
Diamond alipata shavu la kuwa moja ya wahusika katika show hiyo yenye matukio halisi na anakuwa Mtanzania mwingine kuonekana Netflix baada ya Idris Sultan ambaye Machi 26, 2021 alionekana kwenye mtandao huo kupitia filamu ‘Slay’ iliyokutanisha Mastaa wa Afrika kama Ramsey Nouah, Fabian Adeoye Lojede, Simphiwe Ngema, na Amanda Du-Pont.
Filamu nyingine ambazo zinatarajiwa kuanza kuonyeshwa wiki hii ni pamoja na Human Resources, Top boy season 2, Rescued by Ruby,Windfall pamoja na Heist:The great robbery of Brazil Central Bank.