Entertainment

Diamond Platnumz Aingilia Mzozo Kati ya Babalevo na Mbosso

Diamond Platnumz Aingilia Mzozo Kati ya Babalevo na Mbosso

Mzozo ulioshika kasi mitandaoni kati ya Babalevo na Mbosso kuhusu wimbo ‘Pawa’ umechukua mwelekeo mpya baada ya Diamond Platnumz kuingilia kati na kutoa msimamo wake.

Babalevo na Mbosso walikuwa wakijibizana mitandaoni huku jina la Diamond likihusishwa kwenye malumbano hayo. Hata hivyo, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond ametoa kauli ya kutaka pande zote mbili kumheshimu, akisisitiza kuwa amekuwa akiwaheshimu na hana sababu ya kuhusishwa na migogoro yao.

Diamond alimueleza Babalevo kuwa licha ya kumheshimu kama kijana mwenzake, maneno na mienendo yake yameanza kumpa hisia za kutilia shaka, hali inayoweza kupelekea kutojihusisha naye. Aidha, alimkumbusha Mbosso kuwa ana haki ya kukasirika au kujibu pale anapojisikia amekosewa, lakini akamtaka asiingize jina lake katika malumbano hayo, jambo ambalo amesema wameshazungumzia mara kadhaa huko nyuma.

Hitimisho la ujumbe wake lilikuwa wito wa kuheshimiana, akieleza kwamba ikiwa wawili hao wana ajenda tofauti wanazopanga kupitia kivuli chake, basi waendelee, ila yeye hatashiriki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *