Entertainment

Diamond Platnumz apewe elimu ya kodi

Diamond Platnumz apewe elimu ya kodi

Staa wa Bongofleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz  amefanya kikao na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hapo jana katika Ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka hiyo Jijini Dar es salaam na kuzungumza kwa kina pamoja na kupata elimu juu ya kodi.

Mwimbaji huyo ameandika kuhusu kikao hicho leo kwenye ukurasa wake wa Instagram kama ifuatavyo “Kikao kilienda vyema na nikapewa elimu mbalimbali ambazo zitaongeza ustawi bora wa Kampuni na biashara zetu lakini pia namna sahihi ya kuendelea kuchangia pato la Taifa”

“Kipekee nimshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia kwa kutupa Serikali sikivu lakini pia nimshukuru Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu na Kamishna Mkuu TRA Alphayo J. Kidata kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele kwenye kuhakikisha kwamba TRA inaendelea kuwa Mlezi bora kwenye ustawi wa biashara na Wafanyabiashara”

Kikao hiki kimetokana na mahojiano ya Diamond Platnumz Desemba 30, mwaka 2022 ambayo alilalamikia akaunti za Kampuni na zake binafsi kuzuiliwa kutokana na madeni ambayo TRA walisema wanamdai huku akisisitiza kuwa hakupenda jinsi alivyofuatwa kwenye Ofisi za Wasafi kitendo kilichomfanya ajione kama ni Mkimbizi ndani ya Nchi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *