Entertainment

Diamond Platnumz Asema Hana Msemaji Rasmi

Diamond Platnumz Asema Hana Msemaji Rasmi

Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania, Naseeb Abdul Juma, maarufu kama Diamond Platnumz, ametoa tamko rasmi akieleza kuwa hajawahi na hajateua mtu yeyote kuwa msemaji wa maisha yake binafsi au kazi zake za muziki.

Kupitia taarifa hiyo, Diamond amesisitiza kuwa taarifa yoyote inayotolewa na mtu mwingine kwa niaba yake haina uhalali wowote na haitakiwi kuchukuliwa kama ya kweli. Ameeleza kuwa iwapo mtu yeyote ataamua kuamini taarifa hizo zisizo rasmi, basi matokeo ya imani hiyo yatakuwa juu ya mhusika mwenyewe, na yeye hatalaumiwa kwa lolote linalotokana na hilo.

Ameweka wazi kuwa endapo kutakuwa na jambo lolote muhimu la kuzungumza, atazungumza mwenyewe kupitia njia rasmi bila kumtuma mtu yeyote kumwakilisha.

Mashabiki na vyombo vya habari wanahimizwa kufuatilia vyanzo rasmi vya mwanamuziki huyo kwa taarifa sahihi na kuepuka upotoshaji.

Tamko hili limekuja kufuatia hali ya sintofahamu iliyojitokeza kwa muda sasa, ambapo Baba Levo amekuwa akizungumza mara kwa mara kuhusu maisha ya ndani ya Diamond na kazi zake, hali iliyowafanya baadhi ya watu kumchukulia kama msemaji wake wa karibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *