
Staa wa muziki wa Bongofleva Diamond Platnumz ametajwa kuwania tuzo za muziki kutoka Ghana, ziitwazo Ghana Entertainment Awards USA.
Majina ya wanaowania tuzo hizo yalianza kutangazwa, Mei 13 mwaka huu ambapo hadi sasa Diamond anashindania kipengele kimoja kwenye tuzo hizo.
Katika tuzo za Ghana Entertainment Awards USA kwenye msimu wake huu wa nne, Diamond Platnumz anang’ang’ania kipengele cha Best African Entertainer ambacho ni maalum kwa wasanii wote Afrika.
Wanamuziki na watu wengine wanaoshindania kipengele hicho ni Davido, Wizkid, Burna Boy, Tems, Focalistic, na wengine wengi.
Tuzo za Ghana Entertainment Awards USA kwa mwaka huu zinafanyika kwa mara ya nne, na zinatarajiwa kutolewa Julai 8, mwaka 2022 huko jijini New York, nchini Marekani.