Entertainment

Diamond Platnumz Atangaza Msimu wa Pili wa Tamasha la “Diamonds Are Forever”

Diamond Platnumz Atangaza Msimu wa Pili wa Tamasha la “Diamonds Are Forever”

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ametangaza kurejea na msimu wa pili wa tamasha lake kubwa la “Diamonds Are Forever”, kama ishara ya shukrani kwa mashabiki wake kutokana na upendo na sapoti kubwa wanayoendelea kumpa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond amesema ameguswa na mapenzi na uaminifu wa mashabiki wake, akieleza kuwa wamekuwa sehemu muhimu ya mafanikio yake katika muziki.

Msanii huyo anayefanya poa na ngoma yake ya Sasampa, ameongeza kuwa tamasha hilo litakuwa ni njia ya kusherehekea safari yake ya kimuziki na kuwashukuru wote waliomuunga mkono tangu mwanzo.

Tamasha la kwanza la “Diamonds Are Forever” lilifanyika mwaka 2012 katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, na liliweka historia kubwa katika muziki wa Tanzania kwa kujumuisha maonyesho makubwa na maelfu ya mashabiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *