
Staa wa muziki wa Bongofleva Diamond Platnumz amethibitisha kuwa tayari ameshanunua ndege yake binafsi, “Private Jet”.
Diamond amethibitisha hilo kwenye mahojiano yake na DW nchini Ujerumani, akiwa na mtangazaji Josey Mahachie, ambapo alikuwa anamueleza namna staa anavyotakiwa kuishi ili kupata heshima anayostahili.
Diamond amesema yeye ametoka mtaani, ameshanunua magari yenye thamani hadi Shilingi Bilioni 2.3 (Rolls Royce, Black Bedge), anasema inabidi ufanye hivyo, usipofanya hivyo hawatakuona wewe ni wa thamani na sasa tayari ana ndege binafsi.
Itakumbukwa, kwa mara ya kwanza Diamond kueleza mpango wake wa kununua ndege yake binafsi ilikuwa ni miezi miwili iliyopita akizungumza na wanahabari nchini Ivory Coast alipoenda kwenye show yake, ambapo alisema ndege yake hiyo itatua nchini kabla ya mwezi Oktoba.