Entertainment

DIAMOND PLATNUMZ ATILIA SHAKA VIONGOZI WA SANAA TANZANIA

DIAMOND PLATNUMZ ATILIA SHAKA VIONGOZI WA SANAA TANZANIA

Hitmaker wa ngoma ya “Gidi” msanii Diamond Platnumz ameonesha kutoridhika na viongozi wa serikali waliopewa mamlaka ya kusimamia sanaa nchini Tanzania.

Kupitia Instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Diamond ameandika ujumbe unaosomeka ” Serikali ina nia njema sana ya kukuza sanaa ila inatakiwa kuwa makini sana na watu wanaowateua kusimamia nyanja mbalimbali katika tasnia zetu. Maana watu hao wanachokifanya ni kuidhalilisha Taifa na kufanya Taifa letu lionekane halina weledi”

Pamoja na kuandika hayo Diamond Platnumz hajaweka wazi ni viongozi gani ambao amewalenga katika ujumbe wake huo ila walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamehoji kuwa huenda msanii huyo hajafurahishwa na uamuzi wa Shirikisho la Muziki nchini Tanzania kumteua mchekeshaji Steve Nyerere kuwa msemaji wa Shirikisho hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *