Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania, Diamond Platnumz, ametuma salamu za rambirambi kwa wananchi wa Kenya kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu, Raila Odinga.
Kupitia Insta Story Instagram, Diamond ameposti picha yake akiwa anaongea na marehemu Raila wakati wa hafla ya kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi, akielezea masikitiko yake na kumtakia kiongozi huyo pumziko la amani.
Hitmaker huyo wa Nani, ameambatanisha ujumbe wake huo na wimbo wa Zabron Singers uitwao Inaniuma, ishara ya huzuni na uchungu aliouhisi kufuatia kifo cha kiongozi huyo ambaye alimfahamu binafsi.
Diamond alikuwa miongoni mwa wasanii waliotoa burudani wakati wa kampeni za mwisho za Raila mwaka 2022, hafla iliyohudhuriwa na maelfu ya watu. Inadaiwa kwamba msanii huyo alinufaika pakubwa na ushiriki wake katika kampeni hizo, akipokea takribani shilingi milioni 10 za Kenya kwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo kubwa.