Gossip

Diamond Platnumz Awajibu Wakosoaji kwa Begi Lililojaa Dola za Kimarekani

Diamond Platnumz Awajibu Wakosoaji kwa Begi Lililojaa Dola za Kimarekani

Msanii nyota Barani Afrika, Diamond Platnumz, amezua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya hatua yake ya kuonekana kuwajibu wale waliodai kususia muziki wake kutokana na masuala ya kijamii na kisiasa yaliyoibua hisia tofauti miongoni mwa mashabiki.

Kupitia Instagram Story yake, Diamond ameshare video fupi akionyesha begi lililojaa Dola za Kimarekani akiwa ndani ya ndege huku akiambatanisha na wimbo wake wa Sasampa aliyowashirikisha wasanii Focalistic, Uncool MC, Silas Africa, na Xduppy, wote wanatoka Afrika Kusini.

Katika video hiyo, Diamond anaonekana akihesabu maelfu ya dola na msaidizi wake, hatua ambayo imechukuliwa na wengi kama ujumbe wa moja kwa moja kwa wanaodai kususia kazi zake kwa madai ya kujihusisha na siasa zilizotumbukiza Tanzania kwenye machafuko baada ya Uchaguzi mkuu wa Oktoba 29.

Licha ya mjadala huo, Diamond Platnumz anaendelea kubaki miongoni mwa wasanii wenye ushawishi mkubwa barani Afrika, si tu kupitia muziki wake bali pia kupitia miradi yake ya kibiashara. Tu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *