Mwanamitandao aliyegeukia muziki Diana Bahati amemwonya waziwazi mabinti mtandaoni kumuepuka mwanawe, Morgan Bahati, kufuatia mawasiliano ambayo hayakumpendeza kama mzazi.
Katika ujumbe wake, Diana amesisitiza kuwa hana tatizo na mashabiki kumpenda au kuwasiliana na Morgan, lakini amekemea vikali tabia ya wasichana kumwomba hela mtoto wake, akibainisha kuwa lengo lake ni kuhakikisha Morgan anazingatia masomo na malezi mema bila shinikizo au ushawishi wa nje.
Diana, akiwa na msimamo mkali kuhusu malezi na muda wa watoto wake, ametumia mitandao yake kuwakumbusha mabinti hao kuwa Morgan bado ni mwanafunzi na hana uwezo wala wajibu wa kutoa pesa kwa mtu yeyote kwa sasa.
Kauli ya Diana B inakuja mara baada ya binti mmoja kuonekana akimfuata Morgan kupitia mitandao ya kijamii na hata kumwomba pesa.