Entertainment

DIDDY AZINDUA RASMI LEBO YAKE YA MUZIKI

DIDDY AZINDUA RASMI LEBO YAKE YA MUZIKI

Rapa kutoka Marekani P. Diddy amezindua na kuitambulisha Lebo yake mpya ya muziki iitwayo “Love Records” ambayo maalum itasimamia na kufanya kazi na wasanii wa muziki wa R&B pekee.

Lebo hiyo itafanya kazi chini ya ushirikiano na kampuni ya Motown Records.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Diddy amesema ana furaha kuitambulisha lebo hiyo ambayo itafanya kazi na wasanii wapya wa muziki wa R&B pamoja na watayarishaji wenye uwezo mkubwa.

Kwa upande wake ameichukulia kama ukurasa mpya wa maisha yake ya muziki kwani pia ameahidi kurudi kwenye muziki na ataachia Album chini ya lebo yake hiyo.

Mwaka wa 1993 Diddy alianzisha lebo yake iitwayo “Bad Boy Records” na ilipata mafanikio makubwa ikifanya kazi na wakali wa dunia kama marehemu Notorious B.I.G, Faith Evans, 112, Mase, Cassie na wengine kibao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *