
Mwanamuziki kutoka Pwani Dogo Richie amefunguka sababu za wasanii wa Kenya kushindwa kupenya kwenye soko la kimataifa.
Kwenye mkao na waandishi wa habari msanii huyo amesema licha ya wasanii kujikaza kwenye suala la kuachia muziki mzuri, hakuna mazingira rafiki ya kuwawezesha kutanua wigo wa muziki wao kuwafikia wengi kutokana na serikali kutoipa kipau mbele sekta ya muziki ambayo ikipewa uzito huenda ikitangeneza ajira kwa vijana.
Dogo Richie ambaye anahisiwa huenda akaingia ubia wa kufanya kazi na Kaya Records, ametangaza kuwa Jumamosi hii ana jambo lake ambapo amewataka mashabiki wamfuatilia kwa ukaribu kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya kufahamu na kupokea matukio yote kutoka kwake.