
Mwanamuziki kutoka Pwani Dogo Richie kwa mara ya kwanza amekiri kuwa aliwahi kwenda kwa mganga ili amsaidie atoke kimuziki.
Katika mahojiano na Presenter Ali Dogo Richie amesema baada ya kufika kwa mganga aliona kuwa hawezi kumsaidia na tangu kipindi hicho aliacha kuamini kwenye masuala ya kishirikina kwani ndio kikwazo kikubwa cha watu wengi kutoendelea kimaisha.
Hitmaker huyo wa “Tule Sheshe” amewaasa watu kutoamini katika imani za kishirikina na badala yake wamgeukie Mungu wanapokumbwa na matatizo katika maisha.
Lakini pia amenyosha maelezo kuhusu suala la kumtamani kimahusiano malkia wa Tiktok Azziad kwa kusema kuwa ana penzi la kweli kwa mrembo huyo na wala hatafuti kiki kama watu wanavyosema mtandaoni.