Entertainment

Dr. Dre yupo mbioni kuuza haki za nyimbo zake (Master Recording)

Dr. Dre yupo mbioni kuuza haki za nyimbo zake (Master Recording)

Rapa mkongwe na mtayarishaji wa muziki kutoka Marekani, Dr. Dre ameripotiwa kuwa yupo mbioni kuuza baadhi ya haki za nyimbo zake (Master Recording) kwa Kampuni ya Universal Music Group (UMG) pamoja na Kampuni ya Kimarekani ya Shamrock Holdings.

Hata hivyo taarifa za ndani zaidi zinadai, Dr. Dre anauza haki za nyimbo zake zote toka katika LP yake ya kwanza iitwayo “The Chronic” iliyotoka mwaka 1992 pamoja na baadhi ya mirabaha katika utayarishaji na uandishi wa nyimbo zake akiwa na rapa Kendrick Lamar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *