
Msanii aliyegeukia siasa kutoka Uganda Dr. Hilderman amejipata akiwa katika hali ya majonzi baada ya prodyuza aliyekuwa amemuajiri kwenye studio zake za Wokota kukimbia na vifaa vyote vya muziki.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Uganda, prodyuza huyo anayefahamika kama Drainer Beats alitekeleza kitendo hicho cha wizi wa mabavu na kisha akazima simu yake ya mawasiliano.
Hata hivyo jeshi la polisi nchini humo limeanzisha msako wa kumtafuta mtuhumiwa huku chanzo cha prodyuza kutoroka na vifaa vya studio ikiwa hajawekwa wazi.
Ikumbukwe mwezi Oktoba mwaka 2022 Dr. Hilderman alianzisha studios za Wokota kwa nia ya kukuza na kuinua vipaji vya vijana kwenye muziki lakini inaonekana ndoto yake hiyo imekatizwa ghafla na prodyuza Drainer Beats ambaye amemuacha akikadiria hasara ya mamilioni ya fedha.