Entertainment

Dr. Hilderman atangaza ujio wa Album yake mpya

Dr. Hilderman atangaza ujio wa Album yake mpya

Mwanamuziki aliyegeukia siasa kutoka Uganda Dr. Hilderman ametangaza ujio wa Album yake mpya ambayo kwa mujibu wake huenda ikaingia sokoni hivi karibuni.

Kupitia mitandao yake ya kijamii Hilderman amesema Album hiyo ambayo ameipa jina la Favor ina jumla ya ngoma 12 ambazo amezichagua kutoka kwenye maktaba yake ya nyimbo 25 alizozirekodi kwa muda wa miaka miwili.

Licha ya kutoweka wazi wasanii aliowashirikisha kwenye Album yake mpya, Hilderman amesema Album hiyo imekamilika kwa asilimia 100 ambapo amewataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kuipokea kazi hiyo ambayo kwa amehoji kuwa itakuwa ya kitofauti sana kwenye safari yake ya muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *