Entertainment

Drake akuja na mkufu wa Almasi uliotengenezwa kwa Pete za Uchumba 42

Drake akuja na mkufu wa Almasi uliotengenezwa kwa Pete za Uchumba 42

Rapa kutoka Marekani Drake amekuja na mkufu wa Almasi ambao umetengenezwa kwa Pete za Uchumba 42 ambazo aliwahi kutaka kuwavisha wanawake tofauti tofauti kwenye maisha yake lakini akabadili maamuzi.

Sonara maarufu Alex Moss ameiambia Tovuti ya TMZ kwamba mkufu huo unaitwa “Previous Engagements” ikiwa ni kumbukumbu kwa wanawake hao ambao Drake alitamani kuwaoa lakini akabadili gia angani. Alex anasema Pete hiyo imetumia miezi 14 kukamilika na ilitengenezwa kwa mkono huko New York, Marekani. Hata hivyo gharama yake bado haijawekwa wazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *